a) Jibu maswali manne pekee. Swali la kwanza ni la lazima. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja. (mtihani, polisi,kortini) .
b) Ufikapo makutano ya barabara ya Kanduyi, fululiza kulia hadi utakapopata kidaraja. Kisha fuata kichochoro kilicho mkono wa kulia. Hicho kitakufikisha kwa Mganga Musakhulu. (michezoni, mahali, spitalini) .
c) Jaza bilauri maji ya moto. Tia dawa kijiko kimoja cha chai. Yawache yatulie kwa muda wa nusu dakika. Yachuje maji hayo kwenye bilauri nyingine. Dawa hii iko tayari kunywewa. (jikoni, matibabu, kichakani) .
d) Elekeza ncha ya bomba au paipu ya silinda kwenye moto kisha bonyeza kidude kilicho juu ya mtungi. Hakikisha maji ya mtungi hayagusi mwili wako. (kupika, kuogelea, kuzima moto) .
e) Tayarisha vifaa vyote vya kuogesha mtoto. Weka maji fufutende kwa beseni. Mvue mtoto nguo, mwoshe kichwa kwanza, halafu mkalishe ndani ya besini (bafuni, mtoni, uwanjani) .
f) Chemsha maji mpaka yatokote. Tia unga wa mahindi kiasi ndani ya maji moto. Koroga, koroga, songa mpaka sima iive. (resipe, mapishi, ulaji) .
g) Tafadhali fuata foleni vilivyo. Kila mmoja atahudumiwa wakati wake ukifika. (ofisini, msikitini, sokoni) .
h) Egesha gari hapa kwa tahadhari yako. (polisi, shuleni, kituo cha mafuta) .
i) Usioshe kwa maji.Tumia mvuke pekee. (bafuni, nguoni,dobi) .
j) Wekelea mkono wa kulia juu ya msahafu huu, kisha uape. (Kanisani, msikitini, kortini) .