Andika muundo wa kikundi nomino cha sentensi ulizopewa katika nafasi zilizoachwa. Kwa mfano: Msichana mwerevu amefaulu. KN - N+V.
a) Mwanafunzi anacheza KN -.

b) Wewe unaimba vizuri KN -.

c) Ng’ombe wale wamenona sana KN -.

d) Gari la mwalimu limekarabatiwa KN -.

e) Rais na Waziri Mkuu wamewasili KN -.

f) Gege na wasaliti wenzake wamekamatwa KN -.