Tumia viunganishi mwafaka kujaza nafasi zilizoachwa wazi. (Vya uteuzi, vya kuongeza, vya masharti,vya nia/dhamira,matokeo, visababishi,vya wakati , vya nia/dhamira, vya matokeo na vya kinyume).
a) Ukitaka kufika mapema anza safari asubuhi   .

b) Sitanunua sokoni wala dukani   .

c) Wananchi waliondoka baada ya wanasiasa kutoa hotuba yake  .

d) Nitampitia ili nimpatie kitabu chake   

e) Nyaga aliongoza katika mtihani wa kitaifa ijapokuwa alikuwa mgonjwa   .

f) Walimu na wamafunzi walihudhuria mkutano huo   .

g) Kwa vile hakukunyesha wakulima hawakupata mavuno   .