Ngeli ya a-wa

Ngeli hii hujumuisha nomino zote za viumbe wenye uhai kama vile; nomino zinazorejelea binadamu, wanyama, ndege, wadudu na viumbe dhahania au wa kufikirika kama malaika, shetani. Nomino hizi hulazimisha kiambishi awali katika kitenzi kikuu kuwa a katika umoja na wa katika wingi.

Malaika alimchukua na kupaa naye
Malaika waliwachukua na kupaa nao
Askofu wanaongoza maandamano ya amani
Maaskoafu wanaongoza maandamano ya amanai
Mchwa ameonekana katika baraza la nyumba
Mchwa wameonekana katika baraza la nyumba