Kutokana na sifa zifuatazo, dondoa zile zinazobainika katika mazungumzo uliyosoma.
Sifa za misimu.
Lugha iliyotumika katika mazungumzo haya si sanifu k.m poa sana, tuna kwenda hapi n.k.
Hurahisisha mawasiliano miongoni mwa wanaohusika
Huwasaidia wanaohusika kujitambulisha na kikundi maalum.
Huwepo kwa muda tu.
Inapozoeleka huwa sehemu ya lugha ya watu k.m neno matatu.
Huwa lugha ya mafumbo. Kwa wasioelewa misimu, mazungumzo yote ni mafumbo.
Maneno huwa maana nyingi k.m poa, nijichape n.k.
Maneno hugawika katika makundi mbalimbali k.m mazungumzo haya ni ya vijana.